Tanzania emblem
The United Republic of Tanzania

Export Processing Zones Authority

Export Processing Zones Authority

News

Speech from the Minister for Investment, Industry and Trade


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA

Muhtasari wa Hotuba

HOTUBA YA MHESHIMIWA DKT.
ASHATU K. KIJAJI (MB.),
WAZIRI WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023

Dodoma Mei, 2022

1. UTANGULIZI

1. Mheshimiwa Spika, Kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira ambayo ilichambua Bajeti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara tarehe 24, 25 na 28 Machi, 2022, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka 2021/2022. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu likubali kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Kawaida na Miradi ya Maendeleo ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2022/2023.

2. Mheshimiwa Spika, Napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehma kwa kutujaalia waja wake baraka na afya tele na hivyo kutuwezesha kuwa pamoja leo kutekeleza wajibu wetu kwa Taifa. Naomba tuungane sote kumuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutujaza y aliyo mema na kuyapa kibali chake masuala tuliyoyapanga ili yampendeze na yafanikiwe.

3. Mheshimiwa Spika, kwa dhati ya nafsi yangu naomba nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuliongoza Taifa letu kwa ujasiri na uzalendo wa hali ya juu. Ameonyesha utashi mkubwa katika kuvutia uwekezaji kutoka kona zote za Dunia kuja kuwekeza ndani ya Nchi yetu kwa manufaa ya pande zote mbili. Amekuwa ni zaidi ya Mlezi kwa Sekta binafsi akitambua mchango wa sekta hii kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa letu. Mwenyezi Mungu azidi, kumpa afya njema, hekima na busara ili aendelee kulitumikia Taifa letu kwa matokeo makubwa. Aidha, nitumie fursa hii pia ikiwa nawasilisha Hotuba yangu ya kwanza ya Bajeti nikiwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara kumshukuru kwa dhati Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuniamini na kuniteua kuongoza Wizara hii. Hakika ni dhamana kubwa kwangu na nimeipokea kwa moyo mkunjufu. Napenda kumhakikishia Mheshimiwa Rais kuwa, kwa kushirikiana na Naibu Waziri wangu, Viongozi na Watumishi wenzangu wa Wizara na Taasisi zake nitayatekeleza majukumu aliyonikabidhi na kufuata miongozo anayonipatia kwa moyo, uwezo, juhudi na ujuzi wangu wote kwa kushirikiana na Baraza la Mawaziri, Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wote.

4. Mheshimiwa Spika, Napenda kumshukuru Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuchochea maendeleo ya uwekezaji, viwanda na biashara. Pia, namshukuru Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miongozo yake yenye kutia chachu na hamasa katika kuimarisha Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara nchini. Aidha, ninampongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Hotuba yake ya Bajeti iliyowasilishwa kwenye Bunge lako Tukufu tarehe 6 Aprili, 2022. Hotuba hiyo imetoa mwelekeo na dira ya Serikali ya Awamu ya Sita kwa Mwaka 2022/2023 ambapo Wizara yangu itaizingatia katika utekelezaji wake.

5. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi; Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar; na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kuendelea

kusimamia masuala yanayoimarisha Muungano wetu na kuwaletea Watanzania maendeleo. Aidha, namshukuru Mheshimiwa Omar Said Shaban, Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ) na Mheshimiwa Mudrick Soraga, Waziri wa Uwekezaji (SMZ) kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza masuala ya Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

6. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kukupongeza wewe binafsi na Naibu Spika kwa kuchaguliwa kwa kura za kishindo kuliongoza Bunge la Kumi na Mbili (12) la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hiyo inadhihirisha namna Waheshimiwa Wabunge tulivyo na imani kubwa kwenu katika kuliendesha Bunge hili kwa umahiri mkubwa na kuweza kusimamia na kuishauri Serikali ipasavyo.

7. Mheshimiwa Spika, Napenda pia kuipongeza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini, na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Eric James Shigongo, Mbunge wa Buchosa na Waheshimiwa Wajumbe wote wa Kamati hiyo kwa ushauri na umakini wao wakati wa kujadili Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara kwa Mwaka 2022/2023. Ushauri na maelekezo yao yamekuwa msingi muhimu katika kuandaa Hotuba hii ninayoiwasilisha leo. Vilevile, nampongeza Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai, kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha, kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia, nichukue fursa hii kumpongeza, Mheshimiwa Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, kwa kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Nawaahidi kuwapa ushirikiano unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu ya ujenzi wa Taifa letu.

8. Mheshimiwa Spika, Niwapongeze pia Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge, Katibu wa Bunge na Watendaji wote wa Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushirikiano mzuri ambao Wizara na wadau wetu wameendelea kupata. Niwahakikishie kuwa tutaendeleza na kuudumisha ushirikiano huo ili Watanzania wanufaike na matokeo chanya ya utekelezaji wa majukumu ya kisekta.

9. Mheshimiwa Spika, Kupitia kwako ninapenda kutoa shukrani na pongezi kwa Bunge lako Tukufu kwa kazi nzuri ambazo limekuwa likifanya katika kuisimamia na kuishauri Serikali, ikiwemo Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Kupitia kwako, naliomba Bunge liendelee kutupatia ushirikiano ili kuiendeleza Sekta hii ambayo ni msingi mkuu wa ujenzi wa uchumi imara na maendeleo endelevu ya Taifa letu. Aidha, napenda kuwapongeza Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wote kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuongoza Wizara mbalimbali. Kadhalika, niwashukuru Waheshimiwa Mawaziri na Naibu Mawaziri wote kwa ushirikiano wanaonipatia katika kutekeleza majukumu ya kusimamia Sekta hii ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambayo ni mtambuka na inayozigusa Wizara za Sekta zote.

10. Mheshimiwa Spika, Napenda kutumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati wapiga kura wote wa Jimbo la Kondoa kwa imani yao kwangu, kwa kunipa moyo na ushirikiano mzuri ulioniwezesha kuchaguliwa kuwa Mbunge wao na pia katika kutekeleza majukumu yangu kama mwakilishi wao katika Bunge hili. Naishukuru pia familia yangu, ndugu na jamaa kwa dua zao na ushirikiano wao mzuri unaoniwezesha kuwatumikia Watanzania na hususan wawekezaji, wanaviwanda na wafanyabishara bila ya kuchoka. Nawaombeni tuendelee kushikamana ili tufikie malengo tuliyokusudia.

11. Mheshimiwa Spika, Ninaomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi na watendaji wote wa Sekta Binafsi. Kwa uchache, napenda kuwatambua: Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania -TPSF; Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania - CTI; Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania - TCCIA; Baraza la Kilimo Tanzania - ACT; Chama cha Wadau wa Ngozi Tanzania - LAT; Chama cha Wafanyabiashara Wanawake – TWCC; Vikundi vya Biashara Ndogo (VIBINDO); na Taasisi nyingine zote kwa michango yao katika kuendeleza uwekezaji, viwanda, biashara, masoko, viwanda vidogo na biashara ndogo.

12. Mheshimiwa Spika, Nawashukuru pia wamiliki na waandishi wa vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa katika kuelimisha umma wa Watanzania kuhusiana na utendaji wa Wizara, taasisi na uendelezaji wa Sekta zake, kuvutia wawekezaji na kuhimiza uzalishaji viwandani. Nawaomba tuendeleze ari hiyo kwa lengo la kukuza uelewa kwa umma ili washiriki kikamilifu katika kutekeleza masuala ya kuendeleza sekta hii na kutia chachu zaidi katika mafanikio tuliyoyapata.

13. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii ya Bajeti ninayoiwasilisha leo ni matokeo ya uratibu na ushirikiano mzuri wa Viongozi wenzangu katika Wizara, akiwemo Mheshimiwa Exaud S. Kigahe - Mbunge wa Mufindi Kaskazini Naibu Waziri; Prof. Godius W. Kahyarara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara; Dkt. Hashil T. Abdallah, Naibu Katibu Mkuu - Viwanda na Biashara; Bw. Ally S. Gugu, Naibu Katibu Mkuu - Uwekezaji, Wakurugenzi; Wakuu wa Vitengo na Taasisi na Wafanyakazi wote wa Wizara. Napenda kuwapongeza sana na kuwasihi kuendeleza moyo huo wa kujituma katika kuwatumikia Watanzania.

14. Mheshimiwa Spika, Ninapenda kuungana na Viongozi wenzangu kutoa pole kwa Watanzania wote waliokumbwa na kadhia ya kuondokewa na wapendwa wao. Kwa namna ya pekee natoa pole kwa familia na wapiga kura wa Jimbo la Ngorongoro kwa kuondokewa na aliyekuwa Mbunge wao Mheshimiwa William Tate Ole Nasha na Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa.

15. Mheshimiwa Spika, Ninawapongeza Mawaziri wote walionitangulia kuwasilisha na kupitishiwa Bajeti zao za Mwaka 2022/2023 hapa Bungeni. Ni matumaini yangu kuwa mipango na bajeti zilizopitishwa zitaendelea kuwa chachu na kuleta ufungamanisho wenye tija na Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara.

16. Mheshimiwa Spika, Taarifa ya utekelezaji ninayoiwasilisha inabainisha mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, Hotuba hii imeainisha Hali na Mwenendo wa Sekta; Uboreshaji wa Mazingira ya uwekezaji, viwanda na ufanyaji biashara nchini; Mchango wa Sekta katika ukuaji wa Pato la Taifa; Utekelezaji wa Mpango na Bajeti 2021/2022; Changamoto na jitihada za kutatua changamoto hizo; Malengo na Vipaumbele vya Sekta kwa Mwaka 2022/2023; Mwelekeo wa Sekta; na Maombi ya Bajeti ya Mwaka 2022/2023.

17. Mheshimiwa Spika, Baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba kutoa Taarifa ya Utekelezaji wa kazi za Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kwa kipindi cha Mwaka 2021/2022 na Malengo ya Mwaka 2022/2023.

18. Mheshimiwa Spika, Kwa Kumbukumbu ya Bunge, naomba Hotuba yangu yote iingie kwenye Hansard kama ilivyo.

2 HALI NA MWENENDO WA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 18 - 40)

2.1 Uwekezaji

19. Mheshimiwa Spika, Tanzania ina rasilimali nyingi na mfumo wa kitaasisi na kisheria wa kusimamia uwekezaji ambayo inatoa vivutio kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kupitia TIC, EPZA na Wizara za kisekta. Hivyo,uboreshaji wa mazingira ya biashara Nchini na uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali hususan katika miundombinu ya umeme, mawasiliano, maji na usafirishaji kwa njia ya barabara, maji, reli na anga ni kichocheo kikubwa kinachotoa fursa zaidi ya ushiriki wa Sekta Binafsi katika shughuli za uwekezaji na uzalishaji nchini. Miradi mingi iliyosajiliwa italeta fursa nyingi za ajira, mapato ya kodi na yasiyo ya kodi kwa Serikali, kuongezeka kipato cha mtu mmoja mmoja na hivyo kuchangia katika kupunguza umaskini.

2.2 Uwekezaji katika Viwanda

20. Mheshimiwa Spika, Uwekezaji katika Sekta ya Viwanda umeendelea kukua na kumilikiwa kwa sehemu kubwa na Sekta Binafsi na viwanda vingi vinajishughulisha na uongezaji thamani kwa kutumia malighafi za ndani. Aidha, sehemu kubwa ya viwanda hivyo ni vidogo sana ambavyo ni 62,400 (asilimia 77.07), vidogo ni 17,267 (asilimia 21.33), vya kati ni 684 (asilimia 0.84) na vikubwa ni 618 (asilimia 0.76). Kutokana na usajili wa viwanda chini ya TIC na EPZA, inategemewa kuwa viwanda vipya vikubwa 500 vitajengwa kufikia mwaka 2025 na kufanya idadi ya sasa ya viwanda vikubwa vinavyoajiri wafanyakazi zaidi ya 500 kuongezeka kutoka 41 hadi kufikia 541.

21. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imeanza utekelezaji wa Kongani ya Viwanda ya Kwala ambayo uwekezaji wake ni takriban Dola za Marekani bilioni 3 ambayo itakuwa na viwanda 200 vikubwa kwa ajili ya kutengeneza nguo, vifaa vya umeme, vifaa vya ujenzi, dawa na aina nyingine. Awamu ya kwanza itakamilika mwaka 2024 na kutoa ajira za moja kwa moja 100,000 na zisizo za moja kwa moja 300,000.

22. Mheshimiwa Spika, Serikali ikishirikiana na Sekta Binafsi itajenga viwanda katika Maeneo Maalum ya Nala - Dodoma na kongani itakayojengwa katika Mkoa wa Mwanza. Uwekezaji huo utachochea matumizi ya Reli ya Kisasa ya SGR, Bandari za Maziwa Makuu, Bahari pamoja na barabara. Uwekezaji huo utaifanya Tanzania kuwa nguzo ya uchumi ya Bara la Afrika (Africa Economic Power House) na kiunganishi kupitia Bahari - GateWay.

23. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Viwanda Vidogo na vya Kati, jitihada zitakuwa katika ujenzi wa viwanda vidogo vya kisasa vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu ili kuzalisha bidhaa ambazo zinaagizwa kwa wingi kutoka nje ilhali zinaweza kutengenezwa hapa nchini. Viwanda vitaanzia katika Kongani ya Dumila - Morogoro na Kitaraka – Singida ikilenga kukuza teknolojia, kuwezesha nchi kujitosheleza kimahitaji kupitia viwanda vidogo ambavyo uwekezaji wake hautumii mitaji mikubwa, kuongeza fursa za masoko ya mazao na kuondoa utegemezi wa bidhaa za nje.

2.3 Biashara

24. Mheshimiwa Spika, Mauzo ya bidhaa za Tanzania

kwenye soko la China yaliongezeka kwa asilimia 14.31 na kufikia Dola za Marekani Milioni 273.1 mwaka 2021 kutokana na uzalishaji na uuzaji kwa wingi hususan tumbaku, pamba na mbegu za ufuta. Mauzo katika Soko la India yaliongezeka kwa asilimia 90.79 na kufikia Dola za Marekani Milioni 1,008.7 mwaka 2021 kulikotokana na ongezeko la mauzo ya Madini, Korosho, Mbaazi na Maharage ya Soya. Mauzo katika soko la Japan yaliongezeka kwa asilimia 20.97 na kufikia Dola za Marekani Milioni 67.5 mwaka 2021.

25. Mheshimiwa Spika, Mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenda Jumuiya ya Ulaya yalipungua kwa asilimia 41.89. Aidha, Mauzo ya Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 2021 yaliongezeka kwa asilimia 43.73 na kufikia Dola za Marekani Milioni 1,161.2 mwaka 2021 kutokana na ongezeko la mauzo ya chai, mahindi, ngano, alizeti, mchele, bidhaa za karatasi, mabati, vigae, vyandarua, kemikali (methyl bromide), saruji na mafuta ya kupaka. Mauzo ya Tanzania kwenda katika soko la nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika, yalipungua kwa asilimia 10.06 kufikia Dola za Marekani Milioni 1,311.5 mwaka 2021.

2.4 Mwenendo wa Bei za Bidhaa Muhimu Nchini

26. Mheshimiwa Spika, Kumekuwepo upandaji wa bei usioendana na uhalisia katika soko kwa baadhi ya bidhaa hasa zinazoagizwa kutoka nje, katika kipindi cha kuanzia mwezi Desemba, 2021 hususan kwenye bidhaa za ujenzi, vyakula, nishati na pembejeo za kilimo. Kwa m f a n o , w astani wa bei ya Nondo moja ya mm 12 imepanda kwa asilimia 31.8 kutoka Shilingi 20,393 kipindi cha mwezi Machi, 2021 na kufikia Shilingi 26,875 mwezi Machi, 2022. Wastani wa bei ya Bati la geji 30 imepanda k w a asilimia 33.3 na kufikia Shilingi 27,714 mwezi Machi 2022, kutoka Shilingi 20,786 mwezi Machi, 2021. Wastani wa bei ya rejareja ya Saruji kwa mfuko wa kilo 50 imeongezeka kwa asilimia 3.5 kutoka Shilingi 16,125??? mwezi Machi 2020 hadi wastani wa Shilingi 17,662??? mwezi Machi, 2021.

27. Mheshimiwa Spika, Mwenendo wa bei ya mafuta ya kula katika soko la dunia imeendelea kupanda na kufikia mwezi Machi, 2022 wastani wa bei ya mafuta ya alizeti kwa tani moja ilikuwa ni Dola za Marekani 1,491.30 na mafuta asili ya mawese ilikuwa Dola za Marekani 1,776.96 kutoka Dola za Marekani 711.71 na 573.02 kwa tani moja mtawalia kipindi cha mwezi Machi, 2019, sawa na ongezeko la asilimia 149.67.

28. Mheshimiwa Spika, Bei za bidhaa mbalimbali za viwandani hususan zile zinazotegemea malighafi kutoka nje au kuagizwa kutoka nje zikiwemo mafuta ya kula, mafuta ya petroli na ngano zitaendelea kuyumba kutokana na athari za UVIKO-19 na vita ya Urusi na Ukraine na hivyo kuathiri urari wa biashara.

29. Mheshimiwa Spika, Sambamba na kupanda kwa bei za vifaa vya ujenzi na mafuta ya kula, kumekuwa pia na ongezeko la bei za mazao ya chakula Nchini. Kwa mfano, wastani wa bei ya Maharage imepanda kwa asilimia 6.2 kufikia Shilingi 188,294 kwa gunia la kilo 100 Mwezi Machi, 2022. Wastani wa bei ya Mahindi kwa gunia la kilo 100 imeongezeka kwa asilimia 23 na kufikia Shilingi 59,861 Mwezi Machi, 2022. Wastani wa bei ya Mchele kwa gunia la kilo 100 imeongezeka kwa asilimia 33.1 na kufikia Shilingi 185,278 mwezi Machi, 2022

30. Mheshimiwa Spika, Kwa kuzingatia uzito wa jambo hili, Serikali kupitia Wizara yangu, iliratibu na kufanya tathmini ya kina kuhusu suala hili ili kulitafutia ufumbuzi. Tathmini imeonyesha kuwepo kwa visababishi vya upandaji wa bei ya bidhaa hizo ikiwa ni pamoja na:

i) Uwepo wa janga la UVIKO-19 lililosababisha chumi nyingi kufungwa kama moja ya njia ya kukabiliana na ugonjwa huu na hivyo kuzuia bidhaa na rasilimali kuhama kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine;

ii) Vitendo vya baadhi ya wasambazaji wa bidhaa sokoni kupandisha bei, kinyume na makubaliano na Wazalishaji;

iii) Kuongezeka kwa gharama za usafirishaji kunakotokana na ukosefu wa makasha ya kubebea bidhaa (kontena);

iv) Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine pia umeonekana kuathiri mwenenedo wa bei ya baadhi ya bidhaa duniani ikiwemo Tanzania.

31. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto hizi Serikali imeanza kuchukua hatua za muda mfupi na muda mrefu kama ifuatavyo:
i. Kuendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa bei za bidhaa muhimu kwa kushirikiana na wadau na kutafuta vyanzo mbadala vya upatikanaji wa bidhaa hizo ili kukidhi mahitaji;

ii. Kuwaagiza wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa muhimu: Kushusha bei za bidhaa walizopandisha pasipo kuendana na uhalisia wa bei ya soko; Kuuza bidhaa husika kwa kuzingatia gharama halisi za uingizaji, uzalishaji na usambazaji; Kuzalisha na kusambaza bidhaa husika kulingana na uwezo wa viwanda uliosimikwa ili kukidhi mahitaji ya soko;

v. Serikali inawaelekeza wauzaji na wasambazaji wa mbolea zenye bei elekezi wahakikishe wanazingatia bei zilizopangwa na Serikali na wale wote watakaokiuka watachukuliwa hatua kali za kisheria;

vi. Tume ya Ushindani kuendeleakufuatilia kwa karibu mwenendo wa biashara wa bidhaa muhimu ambazo zimeonesha kuathirika zaidi na upandaji wa bei na kuchukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kukiuka Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003.

Vii. Serikali imeendelea kushawishi na kuvutia Wawekezaji wa ndani na nje kwenye uzalishaji wa mazao ambayo tumekuwa tegemezi kwa kiwango kikubwa kutoka nje ya nchi ikiwa ni pamoja na mafuta ya kula, sukari, na ngano. Lengo ikiwa ni kuwa na uzalishaji unaotosheleza mahitaji ya soko la ndani na hatimaye kuuza nje kwa sababu fursa hiyo tunayo kama Taifa.

32. Mheshimiwa Spika, Hata hivyo; Upandaji bei holela usio na msingi wa kufanya hivyo ni jinai na Serikali itachukua hatua. Sheria zipo za kusimamia biashara na kitendo cha kupandisha bei kiholela bila sababu za msingi ni kosa la jinai chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Ushindani Na. 8 ya 2003 (Fair Competition Act, No.8 of 2003). Kwa mujibu wa Kifungu hicho, kupanga bei; kufanya mgomo; kukubaliana katika manunuzi; na kuzuia uzalishaji ni makosa yanayostahili adhabu hiyo.

3 UBORESHAJI WA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para 41 – 46)

3.1 Sera

33. Mheshimiwa Spika, Wizara inafanya mapitio ya Sera ya Taifa ya Uwekezaji ya Mwaka 1996, Sera ya Maendeleo ya Viwanda (1996-2020), Sera ya Viwanda Vidogo na

Biashara Ndogo (2003), Sera ya Taifa ya Biashara (2003) na Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo (2003) ili ziendane na mazingira ya sasa ya uwekezaji na biashara na zipo kwenye hatua mbalimbali za kukamilishwa.

3.2 Sheria

34. Mheshimiwa Spika, Wizara inafanya marekebisho ya Sheria ya Ushindani ya Mwaka 2003; Sheria ya Uwekezaji ya Mwaka 1997; Sheria ya Viwango; Sheria ya Leseni za Biashara;naSheriayaVipimo.Sambambana hilo, Wizara inaendelea na maandalizi ya Kutunga Sheria ya Ahueni ya Athari za Biashara ya Mwaka 2022 (Trade Remedies Act, 2022) ili ziendane na hitaji la Serikali la kuweka mazingira wezeshi ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji nchini.

35. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2021/2022, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, imekamilisha marekebisho ya Sheria ya Makampuni, Sura 212; Sheria ya Majina ya Biashara, Sura 213; na Sheria ya Alama za Biashara na Huduma, Sura 326. Marekebisho yake yamefanyika na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Na.3 ya Mwaka 2021 iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 5 la tarehe 11 Oktoba, 2021.

36. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imefanya marekebisho ya Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni ambapo kwa sasa Sheria hiyo inaruhusu Mwekezaji kuingiza Wataalam hadi 10 kwa masharti nafuu kutoka watano (5) ilivyokuwa kabla ya Mwezi Oktoba, 2021 na kuondoa sharti la kupata ithibati ya vyeti vya elimu kutoka TCU na NACTE kwa wanaoomba vibali vya kazi. Halikadhalika, Serikali imeunganisha Mifumo ya Kielektroniki ya Utoaji wa Vibali vya Kazi kwa Wageni na Wawekezaji (Online Work Permit Application and Issuance System-OWAIS). Mfumo huo umefungamanishwa (integrated) na Mfumo wa Kielektroniki wa Maombi ya Vibali vya Ukaazi (Online System for Application of Residence Permit - e-Permit).

4 MCHANGO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA NCHINI (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 47 - 48)

4.1 Mchango wa Sekta ya Viwanda na Biashara
37. Mheshimiwa Spika, Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.0 ikilinganishwa na asilimia 8.4 mwaka 2020, sawa na upungufu wa asilimia 0.4. Vilevile, Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda ilikuwa asilimia 5.1 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2020 kulikotokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa baadhi ya bidhaa za viwandani. Kwa upande mwingine, Sekta ya Viwanda imetoa ajira 345,615 mwaka 2021 ikilinganishwa na ajira 370,485 mwaka 2020.

38. Mheshimiwa Spika, Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2021 ulikuwa asilimia 8.9 ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2020 sawa na ongezeko la asilimia 0.2. Vilevile, Kasi ya Ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.0 mwaka 2021 ikilinganishwa na asilimia 2.1 mwaka 2020. Ongezeko hilo linatokana na kuongezeka kwa bidhaa zilizouzwa zikiwa ni pamoja na bidhaa za kilimo na bidhaa zilizozalishwa viwandani. Sekta ya Biashara imewezesha ongezeko la asilimia sita (6) la mauzo nje ya bidhaa zenye thamani ya Dola za Marekani 6,755.6 kwa mwaka 2021 ikilinganishwa na Dola za Marekani 6,371.7 kwa mwaka 2020. Ongezeko

hilo limetokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa zisizo asilia hususan bidhaa za viwandani, mazao ya mbogamboga na bidhaa nyinginezo zikijumuisha mahindi na mpunga.

5 UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KATIKA MWAKA 2021/2022 (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 49 - 218)

5.1 Utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2021/2022

39. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ambayo kwa mwaka 2020/2021 imeendeshwa kwa Fungu 11, 44 na 60 ilikuwa na Bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 112.69. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022, Wizara imepokea jumla ya Shilingi bilioni 55.15 sawa na asilimia 48 ya jumla ya Bajeti iliyotengwa. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi bilioni 4.87 kutoka Fungu 11 (sawa na asilimia 69); Shilingi b i l i o n i 31.82 kutoka Fungu 44 (sawa na asilimia 39) na Shilingi bilioni 18.46 kutoka Fungu 60 (sawa na asilimia 76) ya Bajeti zilizotengwa.

40. Mheshimiwa Spika, mchanganuo wa utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2021/2022 ni kama unavyoonekana kwenye uk.30 - 32 wa Kitabu cha Hotuba ya Bajeti.

5.2 Utekelezaji wa Mipango

5.2.1 Sekta ya Uwekezaji

A. Kuboresha Mazingira ya Uwekezaji

41. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na TMEA inatengeneza Mfumo wa Dirisha Moja la Kutoa Huduma kwa Wawekezaji kwa Njia ya Kielektroniki (TeIW) na kufikia Mwezi Machi, 2022, ujenzi ulikuwa umefikia asilimia 90. Katika awamu ya kwanza, mfumo unaunganisha mifumo ya NIDA; Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; BRELA; TRA; na TIC.

42. Mheshimiwa Spika, Wizara imeandaa Kanzidata ya Benki ya Ardhi kwa ajili ya uwekezaji ili kurahisisha upatikanaji wa ardhi ya uwekezaji. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 Kanzidata hiyo ilikuwa na jumla ya maeneo yenye ukubwa wa hekta milioni 1.6 kwa ajili ya uwekezaji. Wizara inaendelea na jitihada za kutafuta ardhi kwa ajili ya uwekezaji kutoka katika Sekta ya Umma na Binafsi.

B. Kuratibu Uwekezaji wa Miradi ya Kimkakati yenye

Manufaa Makubwa

43. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibu uwekezaji katika Kongani Maalum za Viwanda zinazowezesha kupunguza utegemezi wa uagizaji wa bidhaa kutoka nje, kuzalisha ajira kwa wingi na kukuza uchumi.Uwekezaji huo ni pamoja na Kongani ya Viwanda vya Mafuta ya Kula ya mbegu za Alizeti - Kitaraka, Wilaya ya Manyoni, Mkoa wa Singida ambapo ekari 45,000 zimepatikana. Katika Sekta Ndogo ya Sukari, kuna Kongani ya Sukari eneo la Dakawa Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro ambayo wawekezaji wadogo wanaotumia mashine zenye uwezo wa kuchakata tani 200 hadi 500 za miwa kwa siku. Vilevile, katika eneo la Kwala Mkoa wa Pwani, Kampuni ya Sino Tan Kibaha Industrial Park Limited inaendeleza uwekezaji katika kongani lenye ukubwa wa ekari 2,500 ambapo viwanda 400 vinatarajiwa kujengwa na kuwekeza kiasi cha Dola za Marekani bilioni 3, kuzalisha ajira za moja kwa moja 100,000, ajira zisizo za moja kwa moja 300,000 na kuzalisha bidhaa za takriban Dola za Marekani bilioni 6 kwa mwaka. Mradi wa Eneo Maalum la Kiuchumi la Mkulazi lenye ukubwa wa hekta

60,103 limepangwa kwa uwekezaji ambapo hekta 28,000 kwa ajili ya kilimo cha miwa na hekta 32,103 kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine yakiwemo alizeti, mtama na mpunga. Mradi huo utajumuisha Kanda Maalum za Viwanda vya Kuchakata Mazao ya Kilimo. Wizara imesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Symphony Investment Ltd iliyoonesha nia ya uendelezaji wa Mradi huo wakati wa Maonesho ya Biashara ya Expo 2020 Dubai.

44. MheshimiwaSpika,Wizarainaratibuuendelezaji wa Mradi wa Bandari na Kanda Maalum ya Kiuchumi Bagamoyo (Bagamoyo Special Economic Zone – BSEZ). Katika Mwaka 2021/2022, Wizara imeendelea na majadiliano na wawekezaji wa Kampuni za China Merchants Holdings (International) Co. Ltd (CMHI) na Oman Investment Authority (OIA). Majadiliano hayo yanahusu eneo dogo la Mradi wa BSEZ kwa kuendeleza eneo la hekta 3,087 kati ya hekta 9,887 ambapo unahusisha ujenzi wa Bandari (Sea Port) na Kituo cha Usafirishaji (logistics Park) kwenye eneo la hekta 887 na uendelezaji wa Eneo Maalum la Viwanda (Portside Industrial City) kwenye eneo la hekta 2,200. Msingi wa marejeo ya majadiliano hayo ambayo yalisimama mwaka 2018 ni kuhakikisha kuwa Serikali inatekeleza maeneo ambayo ni wajibu wake kama vile ujenzi wa miundombinu wezeshi (barabara, reli, umeme, maji, gesi na mifumo ya mawasiliano) na lango la kuingilia bandarini (dredging) kwa maslahi mapana ya Taifa. Uwekezaji katika maeneo ya Mradi yatafanywa kwa kuvutia wabia wa Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) au kufanywa na mwekezaji binafsi.

C. Kuhamasisha na Kuvutia Uwekezaji

45. Mheshimiwa Spika, Katika hatua za kuhamasisha na kuvutia Wawekezaji nchini; Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ziara katika nchi za Ufaransa, Ubelgiji, Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Marekani na hivyo kutoa mchango mkubwa katika kukuza uwekezaji. Katika ziara hizo, Mheshimiwa Rais aliweka kipaumbele katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini na kueleza jitihada zinazochukuliwa na Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Ziara hizo zilifanikisha kuandaliwa kwa mikutano baina ya wawekezaji na Serikali ikiongozwa na Mheshimiwa Rais, kufanyika kwa makongamano ya uwekezaji na kusainiwa kwa Hati za Makubaliano katika nyanja mbalimbali zilizohusisha sekta ya umma na sekta binafsi.

46. Mheshimiwa Spika, katika ziara ya Ufaransa na Ubelgiji, nchi imefanikiwa kupatikana kwa fedha zitakazoelekezwa katika Sekta za Uchukuzi, kilimo, uchumi wa bluu na Wafanyabiashara wadogo. Hadi kufikia mwezi Machi 2022, Wawekezaji 11 kutoka Ufaransa na wawekezaji sita (6) kutoka Ubelgiji walionesha nia ya kuwekeza nchini. Vile vile kuanzia 3 hadi 6 Mei, 2022 wawekezaji kutoka makampuni 35 kwa uratibu wa Norwegian-African Business Association (NABA) wapo Nchini kwetu katika misheni ya Uwekezaji (Investor mission to Tanzania) wakikutana na viongozi mbalimabali wa Serikali pamoja na Sekta Binafsi kwa ajili ya kutafuta fursa za uwekezaji. Aidha, katika ziara ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), jumla ya Hati za Makubaliano 37 zenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 8 (Sawa na Shilingi Trilioni 18.5) zilisainiwa. Miradi hiyo itazalisha ajira 204,575 katika maeneo ya Mawasiliano, Mafuta na Gesi; Kilimo, Utalii wa Mikutano; Usafirishaji; miundombinu; na viwanda na tayari wawekezaji hao wamekuja nchini kwa ajili ya utekelezaji wa miradi husika. Baadhi ya wawekezaji hao wameshafika nchini katika hatua za awali za kuanza utekelezaji wa mipango yao. Kampuni hizo ni pamoja na

Kampuni ya DP World kwa ajili ya miradi ya Uchumi wa Bluu, Kampuni ya TAQA Arabia kwa ajili ya usambazi wa gesi, Kampuni ya ADNOC kwa ajili ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Kampuni ya Abu Dhabi Future Energy Company kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, Ofisi Binafsi ya Mfalme wa Abu dhabi -Sheikh Ahmed Dalmook Al Maktoum kwa ajili ya kuwekeza kwenye uundaji wa matrekta, utengenezaji wa viuatilifu na pembejeo; na Kampuni ya Symphony Invest ambayo inatarajia kuwekeza kwenye kilimo cha miwa, kiwanda cha sukari na kilimo cha soya katika eneo la Mkulazi.

47. Mheshimiwa Spika, Aidha, ziara ya Marekani ambayo ilijumuisha uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour imewezesha kunadi fursa za uwekezaji nchini na kufanikiwa kuvutia uwekezaji wa Dola za Marekani Trilioni 11.7 katika sekta za kilimo, utalii, biashara, nishati na uchukuzi zitakazozalisha ajira 301.110. Katika Sekta ya Uchukuzi, makubaliano yatawezesha kuwa na usafiri wa ndege wa moja kwa moja kati ya Tanzania na Marekani ambao utachochea utalii, biashara na uwekezaji. Ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Jiji la Dallas ni moja ya hati za makubaliano zilizosainiwa Nchini Marekani, ikiwa na lengo la kuongeza biashara ya bidhaa za Tanzania kupitia Dallas kwenda Bara la Amerika ya Kaskazini na kusini; na kuifanya Tanzania kama lango la kibiashara kwa kuongeza biashara ya bidhaa za Marekani kupitia Tanzania kwenda kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika. Hakika Watanzania tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan; Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mafanikio makubwa anayoiletea nchi yetu kuptia ziara zake anazofanya nje ya Nchi kwani zina athari chanya na matokeo makubwa kwenye Sekta ya uwekezaji na hatimaye kwenye Uchumi wa Taifa letu.

48. Mheshimiwa Spika, V i l e v i l e , Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, miradi 221 ilisajiliwa kupitia TIC na EPZA. Miradi hiyo inatarajiwa kuwekeza mitaji yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 1,922.2 na kuzalisha ajira 45,369. Pia, miradi 77 sawa na asilimia 34.8 inamilikiwa na wawekezaji kutoka nje, miradi 75 sawa na asilimia 33.9 ni ya Watanzania na miradi 69 sawa na asilimia 31.2 ni ya ubia.

49. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TIC imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara kupitia Kituo cha Huduma za Mahala Pamoja ambacho hadi Mwezi Machi, 2022 jumla ya vibali, vyeti na hati mbadala za ardhi 7,734 zilitolewa kwa wawekezaji mbalimbali kupitia Kituo hicho. Wizara kupitia TIC imeanzisha Kituo cha Mawasiliano kwa Wawekezaji (Tanzania Investment Call Centre) ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 mpaka Machi, 2022, jumla ya wateja 916 walifanya mawasiliano kupitia kituo hicho, ili kupata huduma mbalimbali zikiwemo taarifa kuhusu taratibu na upatikanaji wa vibali, usajili, vyeti, taratibu na fursa mbalimbali za uwekezaji.

5.2.2 Sekta ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi

A. Kukuza Maendeleo ya Sekta Binafsi

5 0 . Mheshimiwa Spika, Serikali imejenga uwezo wa uendeshaji wa majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuendesha mafunzo katika Mikoa saba (7) ya Dodoma, Iringa, Manyara, Njombe, Rukwa, Ruvuma na Singida iliyoshirikisha jumla ya washiriki 217 inayojumuisha 129 walitoka Sekta ya Umma na 88 walitoka Sekta Binafsi.

51. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) imeratibu ushiriki wa Sekta Binafsi katika ziara za Serikali (Kenya, BurundinaMarekani)naziarazakikazi(Malawi,Msumbiji na Uganda). Katika ziara hizo, majadiliano yalilenga kutatua changamoto katika kufanya biashara. Aidha, kupitia ushirikishwaji huo, Vikwazo Visivyo vya Kikodi (NTBs) 42 kati ya 64 vilijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na hivyo kuwezesha ustawi wa biashara baina ya Tanzania na Kenya. Katika mafanikio haya pongezi nyingi ziende kwa Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwani haya yote ni matunda ya kazi yake kubwa ya Diplomasia ya Uchumi na majirani zetu lakini na Mataifa yote amabayo tunamahusiano ya kibiashara na kiuwekezaji.

B.Kukuza Ushiriki wa Watanzania katika Miradi ya

Kimkakati na Uwekezaji

52. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi imeendelea kuratibu ushiriki wa Watanzania katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika hapa nchini (Local Content). Katika suala hilo, tunasisitiza maslahi ya Watanzania kwenye maeneo ya ajira, matumizi ya bidhaa za Tanzania, ushiriki wa kampuni za Kitanzania, uhaulishaji wa teknolojia, mafunzo na ushiriki wa jamii kiuchumi. Kwa msingi huo umefanyika ufuatiliaji katika miradi ya Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani Tanga nchini Tanzania, uchimbaji wa madini kwenye migodi yote, miradi ya umeme na maji vijijini, ujenzi wa barabara na madaraja na viwanda vyote vyenye uwekezaji wa kutoka nje.

53. Mheshimiwa Spika, Ufuatiliaji huo umebainisha 21

kuwa, Mwaka 2021, jumla ya ajira 72,395 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja zilizalishwa katika miradi hiyo. Kati ya ajira hizo, ajira 68,305 sawa na asilimia 94.35 zilitolewa kwa wazawa na ajira 4,090 zilitolewa kwa wageni sawa na asilimia 5.65. Aidha, Miradi ya Kimkakati ilitoa kandarasi ndogo ndogo kwa kuingia mikataba na Kampuni 2,019 za Watanzania kwa huduma za chakula, ulinzi, biashara, bidhaa za ujenzi kama vile saruji, nondo, kokoto, mchanga, kampuni za usafiri, kampuni za bima na kampuni za mafuta.

C. Mifuko na Programu za Uwezeshaji

54. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia B a r a z a l a Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) imeendelea kuimarisha uratibu wa mifuko na program za uwezeshaji 62 ili iweze kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo huduma za mikopo, dhamana na ruzuku. Kati ya mifuko na programu hizo, mifuko na programu 52 zinamilikiwa na Serikali na mifuko na programu 10 zinamilikiwa na taasisi binafsi. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 jumla ya mikopo yenye thamani ya Shilingi bilioni 903 ilitolewa kwa wanufaika 5,932,668 kutoka katika mikoa 26 wakiwemo wanawake 3,737,581 na wanaume 2,195,087.

55. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kupitia NEEC imewezesha kuanzisha Vituo vya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi tisa (9) Tanzania Bara katika katika Mikoa ya Dodoma, Geita na Rukwa na hivyo kufikia jumla ya Vituo 17 vilivyoanzishwa katika mikoa sita (6) ya Shinyanga (Kahama), Geita, Singida, Rukwa (Sumbawanga), Kigoma (Vituo 6) na Dodoma (Vituo 7).

Kuendeleza Miradi ya Kimkakati

56. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imefanya utafiti wa Mradi wa Magadi Soda-Engaruka ambapo Upembuzi Yakinifu (Techno-Economic Study) umekamilika kwa asilimia 100. Kazi nyingine zilizokamilika ni pamoja na kufanya tathmini ya Athari za Kimazingira (Environmental Impact Assessment - EIA) iliyochangia upatikanaji wa Cheti cha Mazingira na utafiti wa masoko ya Magadi Soda; Uthamini na uhakiki wa ardhi na mali za wananchi watakaopisha Mradi; Maombi ya leseni 29 kwa ajili ya uchimbaji (Mining Licence) yenye gharama ya Dola za Marekani 58,000; na maandalizi ya kutafuta mwekezaji wa kujenga kiwanda yameanza kwa kuandaa na kukamilisha nyaraka muhimu za kutangaza zabuni.

57. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia NDC imeanza maandalizi ya awali kwa ajili ya kuzalisha mbolea zisizo na kemikali (Bio-fertilizer) kwenye Kiwanda cha Tanzania Bio-tech Product kilichopo Kibaha, Mkoa wa Pwani. Kiwanda hicho kinakamilisha taratibu za kufanya majaribio ya pili ya viuatilifu (Bio pesticides), usajili pamoja na kupata vibali vya uzalishaji wa kibiashara. Uzalishaji wa Viuatilifu utatumia mashine zilizopo kiwandani za kuzalisha viuadudu na kuongeza ufanisi na tija kwenye Kiwanda cha TBPL.

58. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TEMDO pia imekamilisha usanifu na michoro ya mtambo mdogo wa kutengeneza sukari kwa ajili ya wajasiriamali wadogo na utengenezaji (fabrications and manufacture) umeanza. Baadhi ya mashine zinazotengenezwa ni cane crusher, sugar cane juice heaters, sugar cane juice clarifier, vacuum pan evaporator, sugar crystallizer, rotary dryer, na mini boiler. Pia, usanifu wa mashine ya kuandaa mbegu za miwa ili zisishambuliwe na magonjwa (Hot water seed treatment plant) umekamilika na utengenezaji wake unaendelea. Mtambo huo mdogo wa sukari utakuwa na uwezo wa kuchakata tani 10 ya miwa (10 TCH), na kutoa tani moja (1) ya sukari kwa saa moja.

D. Kueneza Dhana ya KAIZEN Nchini

59. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) inatekeleza Mradi wa kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kupitia falsafa ya KAIZEN ambao hapa nchini ulianza kutekelezwa mwaka 2013. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Mradi wa KAIZEN umefanya uhamasishaji wa dhana ya KAIZEN upande wa Pemba kwa wanufaika 80 na upande wa Unguja wanufaika 20.

60. Mheshimiwa Spika, Wizara ilitoa mafunzo ya KAIZEN kwa nadharia na vitendo katika Mikoa ya Kagera, Mtwara, Pwani na Tanga ambapo takriban viwanda 20 vimenufaika na mafunzo hayo na wakufunzi 36 wamepatiwa mafunzo hayo.

G. Uendelezaji na Uzalishaji wa Bidhaa kwa ajili ya

Mauzo Nje ya Nchi

61. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia EPZA kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 imewezesha usajili wa Makampuni mapya 15 ambazo zitaleta jumla ya ajira za moja kwa moja 7,918, Mtaji unaokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 62.8 na mauzo nje yanayokadiriwa kufikia Dola za Marekani milioni 94.85.

B.Uzalishaji Teknolojia kwa Matumizi ya Viwanda

Vidogo na vya Kati

62. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia SIDO inaendelea

kuboresha Vituo vya Kuendeleza Teknolojia (TDC), ambapo katika kipindi cha Mwaka 2021/2022, Vituo viwili (2) vilivyopo katika Mikoa ya Kilimanjaro na Mbeya vinaendelea kufanyiwa maboresho. Aidha, pamoja na maboresho yanayoendelea, Vituo saba (7) vya SIDO vya kuendeleza teknolojia (TDCs) vilivyopo katika Mikoa ya Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Kigoma, Mbeya, Lindi na Shinyanga kwa mwaka 2021/2022, vimeweza kuzalisha mashine 313 na vipuri 1,014 ambavyo viliuzwakwa wajasiriamali. Vituo hivyo pia vinajihusisha na uendelezaji wa teknolojia na kutoa huduma za kiufundi kwa viwanda vidogo na vya kati mjini na vijijini katika mikoa husika kwa kuzingatia Mkakati wa Wilaya Moja Bidhaa Moja (ODOP) na fursa za kimasoko zinazojitokeza.

63. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022 Wizara kupitia SIDO imeweza kutoa mafunzo na ushauri mbalimbali kwa wajasiriamali wahitaji 26,800 katika maeneo ya uendelezaji wa biashara na shughuli za uzalishaji viwandani ambapo wajasiriamali 15,176 walipata mafunzo na wajasiriamali 11,624 walipata huduma ya ushauri.

64. Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa Mikopo kwa wajasiriamali, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Machi, 2022, Wizara kupitia Shirika la SIDO ilikuwa imepokea maombi ya mikopo 3,832 yenye thamani ya Shilingi bilioni 8.327, ambapo jumla ya mikopo 2,166 yenye thamani Shilingi bilioni 4.651 ilitolewa. Kati ya mikopo hiyo asilimia 47 ilitolewa kwa wanawake na kutengeneza ajira 5,321 kati ya ajira hizo 2,714 zilienda kwa wanawake. Aidha, Wizara kupitia SIDO imekuwa ikiwaunganisha wajasiriamali na taasisi za fedha kupata mitaji mikubwa kwa ajili ya shughuli zao za kiuchumi. Vilevile, kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wajasiriamali (SIDO SME - CGS), mikopo yenye jumla ya thamani ya Shilingi milioni 110 ilitolewa katika Mikoa ya Singida na Kigoma.

65. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia BRELA imeendelea kuimarisha na kuboresha Mifumo yake ya Online Registration System (ORS) na Tanzania National Business Portal (TNBP) ambayo hutumika kutoa huduma za kusajili Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Hataza na Leseni za Viwanda na Biashara. Hadi kufikia Mwezi Machi, 2022 BRELA imesajili jumla ya kampuni 7,842 kati ya 11,100 yaliyokusudiwa sawa na asilimia 71. Pia, imesajili Majina ya Biashara 15,034 kati ya 19,500 yaliyopangwa, sawa na asilimia 77 na Alama za Biashara na Huduma 2,872 kati ya 4,500 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 64. Vilevile, BRELA imefanikiwa kutoa Hataza 23 kati ya 35 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 66, leseni za Viwanda 96 kati ya 244 zilizokuwa zimepangwa, sawa na asilimia 39 na leseni za Biashara 8,901 kati ya 13,200 zilizokuwa zimepangwa sawa na asilimia 67.

66. Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha biashara nchini, jumla ya wadau wa biashara 257 katika Mikoa ya Dar es Salaam, Geita na Kigoma walipatiwa huduma ya utatuzi wa changamoto katika Kliniki ya Biashara inayoratibiwa na TANTRADE kwa kushirikiana na Taasisi Wezeshi za Biashara zipatazo 28. Lengo la Kliniki hiyo ni kusogeza huduma karibu na maeneo ya wananchi. Aidha, jumla ya changamoto 479 zinazowakabili wafanyabiashara zilitatuliwa.

67. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TANTRADE ilishirikiana na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kuandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Biashara na Huduma Ndogo Zisizo Rasmi (Wamachinga) katika maeneo mbalimbali nchini. Lengo la Mwongozo huo ni kuwa na usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa biashara ndogo na zisizo rasmi nchini unaotambulika kitaifa ili kukabiliana na changamotozaufanyajibiashara katika maeneo hatarishi katika maeneo mbalimbali mijini. Vilevile, Wizara kupitia TEMDO imekamilisha usanifu wa vibanda bora vya biashara vitakavyowezesha wajasiriamali wadogo kufanya biashara kwenye maeneo maalum yaliyotengwa kwa mpangilio.

68. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC imeendelea kufanyia kazi jumla ya mashauri 15 yanayohusu ukiukaji wa Sheria ya Ushindani ambayo ni: Mashauri matano (5) ya Ukiukwaji wa Sheria ya miungano ya Kampuni bila kuiarifu FCC; Mashauri Matano (5) ya kupanga bei kiholela; na Mashauri matano (5) ya matumizi mabaya ya nguvu za soko (5). Katika mashauri matano (5) yanayohusu miungano ya Kampuni yaliyofanyika bila kuitaarifu FCC, wadaiwa katika mashauri manne (4) waliomba kuyamaliza kwa njia ya suluhu na shauri moja (1) lililobaki lipo katika hatua za awali za uchunguzi. Katika mashauri yanayohusu kupanga bei, wadaiwa katika shauri moja (1) waliiomba FCC kufanya majadiliano kwa lengo la kumaliza shauri hilo kwa njia ya suluhu na mashauri mengine manne (4) yapo katika hatua mbalimbali za uchunguzi. Aidha, katika mashauri yanayohusu matumizi mabaya ya nguvu ya soko, FCC imekamilisha uchunguzi kwenye shauri moja (1) na inaendelea na uchunguzi katika mashauri mengine manne (4).

69. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC ilifanya chunguzi katika masoko mbalimbali ili kubaini mienendo kandamizi na hadaifu. Hivyo, mikataba 264 iliyoandaliwa na upande mmoja (Standard Form Consumer Contracts) ilipitiwa. Kati ya hiyo, mikataba 134 ilipokelewa katika kipindi kilichopita. Mikataba hiyo ilitoka katika Sekta Ndogo za Benki na Fedha. Mapitio ya mikataba hiyo yaliwezesha usajili wa jumla ya mikataba ya watumiaji 35. Jumla ya maombi 229 yanaendelea kushughulikiwa na yapo katika hatua mbalimbali za kupata maamuzi.

70. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia FCC, ilichambua na kupitisha maombi 37 ya miungano ya Kampuni sawa na asilimia 64 ya maombi yaliyoshughulikiwa. Katika maombi yaliyoidhinishwa, maombi 36 yaliidhinishwa bila masharti na ombi moja (1) liliidhinishwa kwa masharti yenye lengo la kulinda ushindani, kukuza uchumi pamoja na kulinda maslahi ya umma katika soko husika. Maombi yaliyoidhinishwa yalilenga kuwezesha kampuni husika kuongeza mitaji kama ilivyofanyika katika Sekta Ndogo ya Benki iliyowezesha benki zilizoungana kukidhi matakwa ya kiasi cha mtaji kinachoelekezwa na Mdhibiti ambaye ni Benki Kuu ya Tanzania; Kuongezeka uzalishaji katika Sekta ya Madini na kuwezesha kampuni husika kuongeza kiasi cha uchimbaji na kuanza kuchimba madini ya aina nyingine tofauti na ya awali mfano machimbo ya Nickel, Mkoani Kagera; Kukuza uchumi wa ndani katika Sekta ya Bima iliyowezesha Watanzania kuwa na hisa katika kampuni husika (local content); na Kuongezeka kwa ufanisi katika uzalishaji katika Sekta ya Kilimo iliyowezesha kampuni husika kupata zana za kisasa katika kilimo.

71. Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia TBS limetoa vyeti vya ubora 60,412 kwa shehena za bidhaa zitokazo nje ya nchi; sawa na asilimia 88.8 ya matarajio ya kutoa vyeti vya ubora wa bidhaa 68,000 kwa mwaka 2021/2022. Aidha, TBS kupitia Programu ya Ukaguzi wa Magari hapa Nchini (Destination Inspection) imekagua magari 31,231 yaliyotumika nje ya nchi na hatimaye kuingizwa nchini sawa na asilimia 69.4 ya lengo la kukagua magari 45,000 kwa mwaka. Vilevile, TBS imetoa taarifa 157 za kitaalam kwa wasafirishaji wa bidhaa nje ya nchi zilitolewa sawa na asilimia 130.6 ya lengo la kutoa ripoti za kitaalam 170 kwa mwaka.

6. MWELEKEO WA SEKTA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 219 - 234)

72. Mheshimiwa Spika, Mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita unalenga kuongeza uwekezaji, kukuza Sekta Binafsi na kujenga uchumi shindani wa viwanda utakaowawezesha Watanzania kufikia na kunufaika na uchumi wa kati wa juu ifikapo 2025. Kufanya hivyo kutawezesha Watanzania kutumia fursa za kiuchumi na kijamii katika mifumo iliyoboreshwa na inayozingatia haki na utawala bora. Ni nia thabiti ya nchi yetu kumfanya kila Mtanzania kuwa na maisha bora na kunufaika na rasilimali na fursa zilizopo na zinazojitokeza. Hivyo, ni jukumu letu sote kuwaandaa na kuwawezesha Watanzania kuchangamkia fursa zilizopo ipasavyo.

A. Kuimarisha Taasisi za Utafiti na Maendeleo ya

Teknolojia na Uwekezaji
73. Mheshimiwa Spika, Katika kuendeleza uchumi wa viwanda, Serikali inaimarisha taasisi zake ili kukidhi mahitaji ya maendeleo na ujenzi wa viwanda nchini. Wizara inaziimarisha Taasisi za Utafiti na Maendeleo ya Teknolojia yaani TIRDO, TEMDO na CAMARTEC kwa kupitia upya na kwa kina majukumu na miundo ya kisheria ya taasisi hizo. Lengo ni kuzifanyia maboresho mahsusi ili ziweze kuwa na tija na ufanisi katika kuleta mwendelezo wa mafanikio ya taasisi hizo na pia kuongeza nguvu katika kuendeleza viwanda nchini.

74. Mheshimiwa Spika, Serikali itajielekeza katika kuimarisha taasisi za uwekezaji nchini hususan TIC, EPZA na NDC ili ziwe mihimili na nguzo zauwekezajikatika viwanda ambavyo ni muhimu katika kujenga uchumi wa Taifa. Msukumo ukiwa ni kujenga viwanda mama, viwanda vya kimkakati na viwanda ambavyo kutokana na umuhimu wake ni vyema Serikali ikashiriki.

B. Kuimarisha taasisi za uwezeshaji Kiuchumi
75. Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu na mchango wa uwezeshaji wananchi katika uchumi na hususan ujenzi wa viwanda vidogo na vya kati, Serikali itachukua hatua za makusudi kuimarisha Mifuko na Programu za Uwezeshaji ili kukuza ujasiriamali nchini. Kipaumbele kitakuwa katika kuimarisha taasisi ya NEEC na SIDO ili ziweze kutoa mikopo kwa wanaviwanda na wafanyabiashara hasa wadogo ili kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja, ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi za aina ya viwanda na bidhaa zinahitajika kutokana na mwenendo wa masoko ya ndani na nje ya nchi.

76. Mheshimiwa Spika, Kwa kutambua umuhimu huo, Serikali itaongeza unafuu wa mikopo inayotolewa na Mfuko wa NEDF. Hivyo, kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 riba za mikopo zitahuishwa ili ziwe chini ya riba za mabenki ya biashara. Viwango vya riba ya mikopo ya uzalishaji itapungua kutoka asilimia 18 hadi asilimia 9. Aidha, riba ya mikopo ya biashara na huduma itapungua kutoka asilimia 22 hadi asilimia 12.

C. Utoaji Huduma kwa Kulenga Wateja
77. Mheshimiwa Spika, Utoaji huduma bora kwa wananchi kwa kiwango kinachoridhisha ni lengo kuu la mabadiliko ya kiutendaji ambayo Serikali ya Awamu ya Sita inayapa kipaumbele. Hivyo, mwelekeo wetu ni kuhakikisha kuwa taasisi za kisekta tukianzia na TIC, TBS, WMA na BRELA zinajielekeza katika kutoa huduma kwa kiwango kinachokidhi matarajio ya wananchi. Wizara yangu na taasisi zake itaongeza ubunifu katika utendaji kazi kwa tija na kutoa huduma kwa weledi ili kuchochea ufanisi katika Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na hatimaye kuongeza Pato la Taifa.

D. Kukuza Maendeleo ya Sekta Binafsi
78. Mheshimiwa Spika, Mtazamo wa Sera za Taifa zinatambua nafasi ya Sekta Binafsi kama injini ya kukuza uchumi. Katika kukuza Sekta Binafsi hasa wajasiriamali wadogo na wa kati, Serikali itaweka mazingira wezeshi na rafiki kupitia upatikanaji wa mitaji, teknolojia rahisi na rafiki, masoko ya uhakika na huduma muhimu zinazolenga kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji ni suala lisilohitaji mjadala. Hivyo, katika kukuza Sekta Binafsi nchini, Serikali itaimarisha majadiliano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji.

79. Mheshimiwa Spika, Kupitia Bunge lako Tukufu, natoa rai kwa Sekta Binafsi kutumia fursa ya uwepo wa mahitaji makubwa ya ngano, mafuta ya kula na sukari kushiriki katika uzalishaji na uchakataji wa mazao hayo nchini ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi na hasa kwenye kuwapokea Wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini kwetu kwa manufaa ya pande zote tatu Serikali; Wawekezaji wa ndani na Wawekezaji wa nje.

E: Kuboresha Mazingira ya Biashara Nchini

80. Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa mazingira bora na endelevu ya biashara ni kichocheo kikubwa na muhimu katika kuvutia wawekezaji wa ndani na nje. Hivyo, Serikali kupitia Wizara yangu itahakikisha kuwa inaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini. Maboresho hayo yatavutia wawekezaji wa ndani na nje katika viwanda na biashara na hivyo kuwezesha kutumia fursa mbalimbali za ndani na nje ya nchi kadri zinavyojitokeza. Misingi ya maboresho ya mazingira ya kibiashara itawekewa nguvu ya kisheria na utaratibu wenye ushirikishaji mpana zaidi wa wadau. Aidha, katika kuhakikisha uendelevu na uhakika wa kuvutia wawekezaji na upatikanaji wa soko kwa bidhaa zetu nje ya nchi, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kutumia Ofisi za Balozi zetu nje ya nchi kutangaza bidhaa zetu ikiwa ni pamoja na kuzishirikisha katika maonesho ya Kimataifa ambayo nchi inashiriki.

E. Ujenzi wa Miundombinu kwa ajili ya Uwekezaji wa

Viwanda

81. Mheshimiwa Spika, Kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya msingi na wezeshi kwa ajili ya ujenzi wa viwanda na ufanyaji biashara ni suala la msingi. Uendelezaji wa miundombinu hiyo kwa kushirikiana na sekta binafsi utapewa msukumo zaidi ili kuleta tija na mvuto kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi. Jitihada za kushirikisha Mamlaka ya Serikali za Mitaa katika kumiliki, kuendeleza na kusimamia Maeneo Maalum ya Uwekezaji nazo zitapewa kipaumbele kabla ya kukimbilia kutafuta wawekezaji wa nje.

82. Mheshimiwa Spika, Maendeleo ya Sekta za Uwekezaji, Viwanda na Biashara Nchini hutegemea uwepo wa maeneo yaliyo na miundombinu stahiki kwa ajili ya uwekezaji ikiwemo nishati ya umeme na gesi asilia, maji, usafiri wa reli pamoja na barabara. Hivyo, Wizara yangu itaendelea kushirikiana na Wizara nyingine kuhakikisha kunakuwa na maeneo ya uwekezaji yenye miundombinu stahiki. Vilevile, Wizara yangu itahakikisha tunapunguza gharama za kuendesha biashara hasa katika utaratibu wa upatikanaji wa leseni na vibali mbalimbali vya biashara, ili kwa pamoja tuweze kuvutia wawekezaji na kukuza Sekta ya Viwanda kwa kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo pamoja na malighafi nyingine ikiwemo madini na mazao ya misitu hivyo kupunguza uuzaji wa mazao na bidhaa ghafi nje ya nchi. Kwa kufanya hivi, Sekta ya Viwanda itaweza kuongeza ajira zitokanazo na uzalishaji viwandani.

F.Kukuza Masoko ya Bidhaa na Huduma zinazozalishwa Nchini

83. Mheshimiwa Spika, Kuthamini rasilimali na bidhaa za ndani ni ukombozi muhimu wa kiuchumi kwa Taifa lolote kwa kuwa, nchi ni soko la kwanza kabla ya kutafuta soko lingine. Suala la msingi ni wananchi kujenga imani na kupata thamani na ubora wanaouhitaji katika bidhaa na huduma za ndani ya nchi. Kwa msingi huo, Wizara itaendelea kuhamasisha uimarishaji wa ubora na matumizi ya bidhaa za ndani, nguvukazi na malighafi za ndani ili kuleta ufungamanisho wa sekta katika kujenga uchumi na kuleta maendeleo kwa wananchi wake. Aidha, Wizara kupitia TANTRADE inaendelea kuhamasisha wananchi kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani kupitia kaulimbiu ya “Nunua Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania’. Kaulimbiu hiyo ni muhimu sana katika kipindi hiki cha ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kuimarisha viwanda vya ndani kwa kutegemea soko la uhakika la ndani ya nchi. Hii itajumuisha kusimamia matumizi ya bidhaa, mazao na nguvukazi ya ndani katika miradi ya kimkakati na uwekezaji unaofanyika nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dhana ya ushiriki wa Watanzania.

84. Mheshimiwa Spika, Wizara pia itaendelea kuhimiza na kuhamasisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu. Wizara itaweka msukumo mkubwa katika kuendeleza kwanza: Viwanda ambavyo sehemu kubwa ya malighafi yake itatoka ndani, hususan kwenye sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, madini na maliasili zilizopo nchini. Viwanda vya aina hiyo vitatupa fursa ya kujenga mfumo wa uzalishaji ndani ya nchi uliofungamana na kushikamana. Pili: Viwanda vya kuzalisha bidhaa ambazo zinatumiwa na watu wengi humu nchini yaani bidhaa kama vile nguo, viatu, mafuta ya kupikia, n.k. Kwa hiyo, viwanda hivyo vitakuwa na uhakika wa soko la ndani kabla ya kufikiria soko la nje. Viwanda hivyo vitatarajiwa kuzalisha ziada kwa ajili ya masoko ya nje na hivyo kutuongezea akiba ya fedha za kigeni.

G. Kujenga Sekta Binafsi
85. Mheshimiwa Spika, Katika kufanikisha na kuimarisha soko la ndani, tunahitaji kuwa na Sekta Binafsi imara ambayo inaakisi utashi wa kisera na malengo ya kitaifa. Hivyo, pamoja na haki ambayo Sekta Binafsi inastahili, ina wajibu wa kutekeleza majukumu ambayo yana tija na kuweza kuendeshwa kibiashara ikiwemo kulipa kodi na ada stahiki za Serikali. Kwa upande wa wawekezaji kutoka nje, ni jukumu na wajibu wao kuhakikisha kuwa wanazingatia mikataba na masharti ya uwekezaji ikiwemo kuwajibika kulipa kodi na ada zinazostahiki kwa Serikali, kulipia michango ya wajibu kwa nchi, kujenga mahusiano mema katika maeneo ya uwekezaji na kuzingatia ushiriki wa Watanzania (matumizi ya bidhaa, wafanyakazi, malighafi, huduma za ndani, nk).

86. Mheshimiwa Spika, Kwa upande mwingine, wawekezaji wa ndani wanakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo ukosefu wa mitaji, matumizi ya teknolojia duni, upatikanaji wa ardhi, upatikanaji wa masoko na ujuzi stahiki katika shughuli za uzalishaji viwandani na kuendesha biashara. Kimsingi, Sekta hiyo inahitaji kulindwa kwani viwanda vingi ni vidogo na vichanga kukabiliana na ushindani wa nguvu za soko na viwanda ambavyo tayari vimelindwa vya kutosha na kujijengea uwezo mkubwa wa ushindani. Ulinzi huo tunaozungumzia kwa viwanda vyetu pia ulikuwa

ukifanywa na nchi zilizoendelea kiuchumi zikiwemo China na India kwani biashara na uwekezaji katika eneo hilo la wazalishaji, wafanyabiashara na wawekezaji kwa sehemu kubwa ni wadogowadogo. Azma ya Serikali sio kulinda shughuli za uzalishaji zisizo za tija bali ni kuhakikisha shughuli zenye tija zinaimarika na kuweza kushindana kimataifa.

7 VIPAUMBELE KWA BAJETI YA MWAKA 2022/2023 (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 235 - 236)

87. MheshimiwaSpika,Katika Mwaka 2022/2023, Vipaumbele vikuu vya Wizara ni:

8

i. Kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kipaumbele iliyopo katika Mpango na Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2020;

ii. Uwekezaji katika Kongani na maendelezo kwenye SEZ, EPZA, Kongani za viwanda Mfano - Kongani ya Kigamboni, Kwala na Kitaraka;

iii. Usimamizi na udhibiti wa masoko;
iv. Ushiriki katika shughuli za Kikanda EAC, SADC,

AfCFTA na Kimataifa;
v. Kuondoa urasimu katika kuhudumia wawekezaji na

wafanyabiashara; na
vi. Kuimarisha ushiriki wa Sekta Binafsi moja kwa

moja katika uchumi na uwezeshaji wa wananchi.

MALENGO YA MWAKA 2022/2023 (Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 237 - 243)

8.1.1 Maendeleo ya Uwekezaji

88. MheshimiwaSpika,Katika Mwaka
2022/2023, Wizara itatekeleza malengo yanayojielekeza katika Kuhamasisha uwekezaji; kusimamia maendeleo ya Sekta Binafsi, maendeleo ya viwanda, maendeleo ya biashara na masoko na uendelezaji wa ujasiriamali.

9 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023

(Rejea Kitabu cha Hotuba ya Bajeti Para ya 260 - 261)

9.1 Makisio ya Maduhuli kwa Mwaka 2022/2023

89. MheshimiwaSpika,Katika Mwaka 2022/2023, Wizara inatarajia kukusanya maduhuli ya Shilingi 6,000,000 kutokana na uuzaji wa nyaraka za zabuni.

9.2 Maombi ya Fedha kwa Mwaka 2022/2023

90. MheshimiwaSpika,ili Wizara iweze kutekeleza majukumu na malengo yaliyopangwa, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu liridhie na kupitisha makadirio ya Shilingi 99,105,506,000 katika Fungu 44 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na Taasisi zake kwa mwaka wa Fedha 2022/2023 kwa mchanganuo ufuatao:

  1. i) Shilingi 68,308,687,000 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Shilingi 8,728,788,000 ni za Matumizi Mengineyo (OC) na Shilingi 59,579,899,000 ni kwa ajili ya Mishahara;
  2. ii) Shilingi 30,796,819,000 ni za Matumizi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo Shilingi 30,346,819,000 ni fedha za ndani na Shilingi 450,000,000 fedha za nje.

9.3 HITIMISHO

91. Mheshimiwa Spika, Naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru tena Watanzania wote na hasa Wazalendo

wa Nchi hii kwa kuendelea kutuunga mkono katika jitihada zetu za kuendeleza Sekta ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara. Katika kipindi kilicho mbele yetu, tutaendeleza jitihada za kujenga na kuimarisha misingi thabiti ya uchumi kwa kuvutia wawekezaji na ujenzi wa viwanda kama ilivyobainishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Ni jukumu kubwa ambalo linapaswa kuendelea kuungwa mkono na wapenda maendeleo wote na hasa Watanzania na wazalendo wote. Tunahitaji kila Mtanzania popote alipo kutimiza wajibu wake, kujituma, kubadilisha mtizamo na kuwa mstari wa mbele kulinda na kutetea jitihada na kuendeleza uwekezaji, viwanda na biashara kwa maslahi ya nchi yetu. Inawezekana, tutimize wajibu wetu.

92. MheshimiwaSpika, kwa mara nyingine naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii pamoja na vielelezo vyote inapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara www.mit.go.tz

93. Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja.